Search a title or topic

Over 20 million podcasts, powered by 

Player FM logo

Rfi Kiswahili Podcasts

show episodes
 
Artwork

1
Habari RFI-Ki

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Weekly+
 
Makala ya kila siku yanayompa fursa msikilizaji kutoa maoni yake juu ya habari zilizopewa uzito wa juu kwa siku husika. Msikilizaji hushiriki kwa kutuma ujumbe mfupi pamoja na kupiga simu.
  continue reading
 
Artwork

1
Jukwaa la Michezo

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly+
 
Makala haya yanaangazia maendeleo ya michezo mbalimbali Ulimwenguni na pia huwa haiwaweki kando wanamichezo waliobobea na vilevile kufanya uchanganuzi wa kina wa michezo wakati wa mashindano mbalimbali.
  continue reading
 
Artwork

1
Wimbi la Siasa

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly+
 
Makala ya Wimbi la Siasa inakupa fursa ya kufahamu masuala ya kisiasa yanayoendelea ndani na nje ya Bara la Afrika. Kwenye Makala haya utapata habari ambazo zinakugusa moja kwa moja wewe msikilizaji. Kila wakati usikose kusikiliza Makala ya Wimbi la Siasa
  continue reading
 
Ni Makala yanayoangazia kwa jicho la tatu mazingira halisi ya dunia yalivyo bila kusahau kile ambacho kinachangia kuyaharibu. Utapata kufahamu namna ambavyo mazingira na rasilimali zinavyoharibiwa huku pia teknolojia ikijumuishwa. Hakika mazingira mazuri ya leo ni dunia yako kesho.
  continue reading
 
Artwork

1
Siha Njema

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Weekly
 
Makala inayojadili kwa kina masuala ya afya, tiba na kutambua magonjwa mbalimbali bila ya kusahau namna ya kukabiliana nayo. Watalaam walibobea kwenye sekta ya afya watakujuvya na kukuelimisha juu ya umuhimu wa kuwa na afya bora na si bora afya. Pia utawasikiliza kwa maneno yao watu ambao wameathirika na magonjwa mbalimbali na walikumbwa na nini hadi kufika hapo walipo.
  continue reading
 
Artwork

1
Jua Haki Zako

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Weekly
 
Jua Haki Zako ni makala yanayokuelimisha juu ya umuhimu wa kufahamu haki zako na sheria halali zilizomo kwenye jamii, mataifa na dunia kwa ujumla. Jua Haki Zako itakuelimisha juu ya masuala mbalimbali ya kisheria ndani ya Afrika Mashariki, Afrika na Duniani kwa ujumla.
  continue reading
 
Artwork
 
Fahamu masuala kadha wa kadha kuhusu uchumi kama vile, namna ya kupambana na umaskini, mfumuko wa bei, kushamiri kwa matumizi ya dola na athari za kuyumba kwa uchumi wa dunia kwa nchi za Afrika. Mada hizi zinafanyiwa utafiti wa kina na zinazungumzwa kwa lugha rahisi inayoeleweka ili kukufanya uelewe na usichoke kusikiliza .
  continue reading
 
Changu Chako, Chako Changu ni makala inayozungumzia masuala ya historia, utamaduni, muziki na lugha ya Kifaransa Afrika Mashariki na Kati na duniani. Makala haya yatakuhabarisha pia kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ya Watu Wanaotumia lugha ya Kifaransa kwenye Mawasiliano (L'OIF) na jinsi gani kujifunza na kuelewa lugha nyingine inaweza kuimarisha mahusiano kwenye sehemu zote za maisha ya binadamu.
  continue reading
 
Artwork

1
Nyumba ya Sanaa

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly+
 
Nyumba ya Sanaa ni Makala ya Utamaduni ambayo inatoa fursa kwa wasanii na wadau wa sanaa kuwasilisha maoni yao kwa ajili ya maendeleo ya kweli ya Afrika na dunia kwa ujumla, tukiwa na lengo la kudumisha na kuendeleza tamaduni nzuri katika mwingiliano wa tamaduni uliopo, tukizingatia maisha ya kisasa na utandawazi kwa ujumla.
  continue reading
 
Artwork

1
Mjadala wa Wiki

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly
 
Huu ni wasaa wa kukutana na wageni mbalimbali watakaokuwa wakifika katika studio zetu na kuzungumza moja kwa moja yaani LIVE. Ni mjadala wa kila Jumatano asubuhi ambao utagusa masuala muhimu yanayoibuka ndani na nje ya Bara la Afrika katika nyanja tofaut itofauti. Mjadala wa wiki ni wasaa utakaokuzungusha dunia nzima kupitia mawimbi ya RFI Kiswahili.
  continue reading
 
Artwork

1
Talisman Brisé

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly
 
Talisman Brisé ni tamthilia ya redio inayosimulia hadithi ya mtunza bustani Kwame ambaye bosi wake Profesa Omar anatekwa nyara na watu wasiojulikana. Kwa nini Profesa Omar anatekwa nyara na watu hao? Mfanyakazi wake Kwame atafanikiwa kumuokoa Bosi wake? Fuatilia haya kwenye tamthilia ya Talisman Brise hapa rfi kila siku ya jumapili ndani ya Makala ya Changu Chako Chako Changu.
  continue reading
 
Artwork

1
Muziki Ijumaa

RFI Kiswahili

icon
Unsubscribe
icon
icon
Unsubscribe
icon
Monthly
 
Makala ambayo inakupa nafasi ya kujua masuala mbalimbali ya Muziki na Burudani. Ndani ya makala haya utapata taarifa za wanamuziki, historia zao na bila kusahau mahojiano na wanamuziki mbalimbali. Hii ni fursa ya pekee kwa wasikilizaji kujiliwaza baada ya kazi za juma zima kupitia burudani ya muziki. Makala ya muziki ijumaa pia itakuwezesha kufahamu wasanii kutoka sehemu mbalimbali duniani na kujua wanafanya nini.
  continue reading
 
Loading …
show series
 
Mafuta ya mzeituni, alizeti, mafuta ya nazi,mafuta ya mawese ni baadhi ya mafuta kula ambayo yanapendekezwa kutokana na namna yanavyotengenezwa. Mengi hutengenezwa kwa kukamuliwa ,bila kuongezwa kemikali bila kutumia joto,hivyo ubora wake ni wa juu. Mafuta haya hata hivyo ni ya bei juu sana na watalaam wanashauri badala ya kuchagua mafuta ambayo si…
  continue reading
 
Djibouti limekuwa taifa la hivi punde kuondoa rasmi kikomo cha umri wa rais , hatua inayotoa fursa kwa rais Ismail Omar Guelleh kugombea muhula wa sita katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Aprili mwaka ujao. Awali Katiba ya nchi hiyo ilikuwa inamzuia rais kugombea tena baada ya kufikisha miaka 75. Hali hii pia imeonekana kwenye mataifa kadhaa ya Af…
  continue reading
 
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na waamuzi watatu nchini Rwanda kusimamishwa kwa muda, Kongamano la nne la Kibiashara la Soka lakamilika nchini Kenya, awamu ya mwisho ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa kina dada, tuzo za CAF mwaka huu, mechi za kufuzu hatua ya makundi michuano ya Klabu Bingwa Afrika, mkenya Ruth Chepngetich apigwa marufuku ya m…
  continue reading
 
Katika makala haya shaba yetu inalenga nchini DRC hasa eneo la Mashariki, ambapo tunajadili haki za malemavu eneo hilo. Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, mamia ya watu wenye ulemavu wamejikuta wakihangaika kuokoa maisha yao, kipindi hiki vita vikiendelea kusheheni eneo hilo. Miji kama Goma, Rutshuru na Sake imeshuhudia maelfu wakikimb…
  continue reading
 
Hatua ya rais wa Kenya William Ruto kumtunuku aliyewahi kuwa waziri Mkuu na kiongozi wa upinzani nchini Kenya, hayati Raila Odinga, nishani ya juu zaidi nchini, kukamatwa kwa makamu mwenyekiti wa chama cha Chadema nchini Tanzania, John Heche, DRC na Rwanda zakubaliana juu ya mchakato wa upatikanaji wa amani chini ya upatanisho wa Marekani, uchaguzi…
  continue reading
 
Viongozi wa dunia, wataalam wa Afya na wanasayansi wanakutana Afrika Kusini siku chache kabla kikao cha G20, ili kuanganzia kuhusu njia za kufadhili afya bila kutegemea ufadhili wa kigeni.Tumemuuliza msikilizaji maoni yake kuhusu uwezo wa mataifa ya Afrika kufadhili miradi ya afya?By RFI Kiswahili
  continue reading
 
Miongoni mwa matukio makubwa yaliyojiri wiki hii ni pamoja na wakenya kuomboleza kifo cha mwanasiasa mashuhuri aliyewahi kuwa waziri mkuu wa nchi hiyo Raila Amolo Odinga, kuzinduliwa kwa jukwaa jipya la kisiasa : Okoa DR Congo, kuendelea kwa kampeni za kisiasa kuelekea uchaguzi mkuu kule Tanzania, kuapishwa kwa kiongozi wa kijeshi wa Madagascar, na…
  continue reading
 
Kuanzia yale ya nazi hadi mizeituni, mboga hadi kanola, parachichi hadi mafuta ya wanyama maswali yameibuka kuhusu tunajuaje yapi mazuri ya kutumia, na ikiwa tunapaswa kuepuka yoyote yale kabisa Watalaam wa afya wanahoji mafuta ni kiungo muhimu katika mwili wa binadaam kwa kuwa huchangia madini muhimu na pia husaidia utendakazi wa viungo muhimu mwi…
  continue reading
 
Hivi leo viongozi wa dunia akiwemo rais wa Marekani, Donald Trump, wanakutana Misri kujadili mustakabali wa eneo la Gaza, baada ya makubaliano ya kihistoria ya wiki iliyopita. Makubaliano haya yameshuhudia kuachiwa kwa mateka, wafungwa na kusitishwa kwa vita vya Gaza. Tunakuuliza, unaamini makubaliano kati ya Hamas na Israel safari hii yatadumu?Nin…
  continue reading
 
Karibu katika makala ya leo Jumapili Changu Chako Chako Changu ambapo leo nakuletea sehemu ya pili ya siku ya kimataifa ya ukalimani na tafsiri, na kwenye le parler francophone nitakujuwa kinachoendelea kwenye vituo vya Alliance Francaise za Ukanda na kwenye Muziki nitakuletea mwanamuziki Mace Ice. Mimi ni Ali Bilali mtangazaji wako asiependa makuu…
  continue reading
 
Tuliyokuandalia leo ni pamoja na tathmini ya timu za Afrika ambazo zimefuzu Kombe la Dunia 2026 na ni nani ambao wana nafasi ya kufuzu kuelekea raundi ya mwisho ya mechi za kufuzu, FIFA yateua wajumbe kutoka CECAFA, Herita Ilunga ndiye mkurugenzi mpya wa FECOFA nchini DRC, kocha wa zamani wa Yanga Nassredine Nabi waachana na Kaizer Chiefs, nyota ta…
  continue reading
 
Habari kuu wiki hii ni pamoja Israel kuanza kuwaondoa wanajeshi wake kwenye baadhi ya maeneo ya Gaza, rais wa Ufaransa amteua tena Sebastien Lecornu kuwa waziri mkuu huku kukiwa na mvutano wa kisiasa, rais wa DRC, Félix Tshisekedi, amtaka mwenzake wa Rwanda, Paul Kagame, kuwaamuru waasi wa M23 kuacha vita mashariki mwa Congo, siasa za kikanda, yali…
  continue reading
 
Msikilizaji kesho Ijumaa oktoba 10 kamati inayotoa tuzo za kimataifa za Nobel itamtangaza mshindi, wakati huu watu wengi wakiwa wamempendekeza rais wa Marekani Donald Trump kutokana na mchango wake wa kutafuta amani mashariki ya kati, hata hivyo wadadisi wanasema kiongozi huyo hawezi kupewa tuzo hiyo. Unafikiri ni Kiongozi gani anastahili kupewa tu…
  continue reading
 
Habari rafiki ya jumatano octoba 08 imeangazia vitendo vya utekaji nyara ambavyo vimeongezeka katika nchi za ukanda wa Afrika mashariki, hivi karibuni nchini Uganda wanaharakati wawili kutoka nchini Kenya walikamatwa baada ya kuhudhuria mkutano wa kisiasa wakati nchini Tanzania, aliyekuwa balozi wa nchi hiyo huko Cuba Humphrey Polepole alitekwa na …
  continue reading
 
Wachambuzi wa mambo wanaona kuwa waasi wa AFC/M 23 wanaendelea kujiimarisha zaidi kisiasa na kiuchumi, katika maeneo wanayodhibiti, Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, licha ya kuwepo kwa mkataba wa Washington uliokubaliwa kati ya DRC na Rwanda kuhusu namna ya kupata mwafaka wa kudumu. Hatua hii inamaanisha nini ? Tunachambua.…
  continue reading
 
Loading …
Copyright 2025 | Privacy Policy | Terms of Service | | Copyright
Listen to this show while you explore
Play